Hebroni: Makala
Habari Mpya
Loading...
Showing posts with label Makala. Show all posts
Showing posts with label Makala. Show all posts

Wednesday, February 3, 2016

The Swedish Church to Collect '39' Million to Build a Mosque

For years the Swedish church parish in Nacka has with an ongoing project planned to build a mosque adjacent to the existing church in Fisksätra in Stockholm. 

The project to build the joint building, called "House of God" is estimated to cost SEK 39 million ($4,548,630), an amount the church tries to collect through a foundation. 

Critics have naturally questioned whether the church really should be building mosques, or instead focus on the Christian faith.

Plans to build the "House of God" in Fisksätra, Nacka municipality in southern Stockholm, began already in 2009. Fisksätra is an ethnic community with a large Muslim populations. The following year, priest and former bishop of Karlstad, Bengt Wadensjö, presented the project in an article in the Swedish newspaper Svenska Dagbladet. He referred to the Sweden Democrats:

Swedish church to collect 39 million to add a mosque- When fear of the unknown in the form of Islam now gives Sweden a profile in the news by SD taking place in parliament, I want to highlight a different picture of Sweden. Jimmie Åkesson (head of SD) wrote in Aftonbladet, October 20, 2009, that "Muslims are our biggest foreign threat". In Nacka we do not believe that immigrants or Muslims would be a threat. They are an asset."

Bengt Wadensjö said that Muslims and Christians should unite in the idea that God is one, and added that "Muslims are generally peaceful and honest", and that the project would lead to that "world peace begins in Fisksätra".

Concretely, the idea is that the mosque will be built next to the church and the two united by a glazed foyer. The Muslim community have been allowed to buy the land needed for SEK 300,000, an amount that will not be paid until the project is complete.

In November 2014, Nacka Parish decided to transfer bequeathed funds to the collection fund to build the mosque, ie money from deceased who wanted to support the Swedish Church by donating money. Although this decision was appealed, the protest was rejected.
Read more »

Sunday, January 31, 2016

“Heri Mtu Yule Aonaye Hekima”

ALIKUWA mshairi, msanifu wa majengo, mfalme. Akiwa na pato la dola za Marekani zaidi ya milioni 200 kwa mwaka, ndiye aliyekuwa mfalme tajiri kuliko wafalme wote duniani. Mtu huyo pia alikuwa maarufu kwa hekima yake. Malkia mmoja aliyemtembelea alivutiwa sana na kusema hivi kwa mshangao: “Tazama, sikuambiwa nusu; wewe umezidi kwa hekima na kufanikiwa kuliko habari nilizozisikia.” (1 Wafalme 10:4-9) Hiyo ndiyo iliyokuwa hadhi ya Mfalme Solomoni wa Israeli la kale.
Solomoni alikuwa na utajiri na hekima pia. Hali hiyo isiyo ya kawaida ya kuwa na utajiri na hekima ilimfanya Solomoni aweze kuchanganua na kuamua ni nini kilichokuwa muhimu zaidi. Aliandika hivi: “Heri mtu yule aonaye hekima, na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye ana thamani kuliko marijani, wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.”—Mithali 3:13-15.
Ingawa hivyo, hekima yaweza kupatikana wapi? Kwa nini ni yenye thamani zaidi kuliko mali? Ni mambo gani yenye kuvutia kuhusu hekima? Sura ya 8 ya kitabu cha Biblia cha Mithali, iliyoandikwa na Solomoni, yajibu maswali hayo kwa njia yenye kuvutia. Katika sura hiyo hekima yafananishwa na mtu, kana kwamba inaweza kuzungumza na kutenda. Na hekima yaonyesha jinsi inavyovutia na vilevile thamani yake.
“Anapiga Kelele”
Sura ya 8 ya Mithali yaanza kwa swali lisilohitaji jibu: “Je! hekima halii? ufahamu hatoi sauti yake?”* Naam, hekima na ufahamu waendelea kulia, lakini kwa njia iliyo tofauti kabisa na mwanamke asiye na maadili anayeotea mahali penye giza na kumnong’onezea maneno ya utongozi kijana asiye na ujuzi. (Mithali 7:12) “Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, penye njia panda, ndipo asimamapo. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele.” (Mithali 8:1-3) Sauti kubwa na ya ujasiri ya hekima yasikika kwa nguvu na waziwazi mahali pa umma—malangoni, penye njia panda, mahali pa kuingia mjini. Watu wanaweza kusikia sauti hiyo kwa urahisi na kuitikia.
Ni nani awezaye kukana kwamba karibu kila mtu duniani anaweza kupata hekima ya Mungu iliyo katika Neno lake lililopuliziwa, Biblia? “Biblia ni kitabu ambacho kimesomwa na watu wengi zaidi katika historia,” chasema kichapo The World Book Encyclopedia. Chaongezea hivi: “Biblia ndiyo imegawanywa kwa wingi zaidi kuliko kitabu kingine chochote. Biblia imetafsiriwa pia mara nyingi zaidi, na katika lugha nyingi zaidi, kuliko kitabu kingine chochote.” Kwa kuwa Biblia nzima au visehemu vyake vyapatikana katika lugha na lahaja zaidi ya 2,100, zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaweza kusoma angalau sehemu fulani ya Neno la Mungu katika lugha yao wenyewe.
Mashahidi wa Yehova wanatangaza hadharani ujumbe wa Biblia kotekote. Katika nchi 235, wanahubiri kwa bidii habari njema za Ufalme wa Mungu na kufundisha watu kweli inayopatikana katika Neno la Mungu. Nakala zaidi ya milioni 20 hugawanywa za majarida yao yanayotegemea Biblia ambayo ni Mnara wa Mlinzi, jarida linalochapishwa katika lugha zaidi ya 140, na Amkeni! jarida linalochapishwa katika lugha 83. Bila shaka, hekima inaendelea kupiga kelele katika mahali pa umma!
“Sauti Yangu Ni kwa Wanadamu”
Hekima inayofananishwa na mtu yaanza kwa kusema hivi: “Enyi watu, nawaita ninyi; na sauti yangu ni kwa wanadamu. Enyi wajinga, fahamuni werevu, nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu.”—Mithali 8:4, 5.
Mwito wa hekima unawafikia wanadamu kila mahali. Unaalika wanadamu wote. Hata wale wasio na uzoefu wanaalikwa kujipatia werevu, au busara, na wapumbavu wapate uelewevu. Kwa kweli, Mashahidi wa Yehova wanaamini kwamba Biblia ni kitabu kwa ajili ya watu wote nao hujitahidi pasipo ubaguzi wowote kutia moyo kila mtu wanayezungumza naye kuichunguza na kupata maneno ya hekima yaliyomo.
‘Kinywa Changu Husema Kweli’
Ikipanua mwaliko wake, hekima yaendelea kusema: “Sikieni, maana nitasema yaliyo mazuri, na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili. Maana kinywa changu kitasema kweli, na uovu ni chukizo kwa midomo yangu. Maneno yote ya kinywa changu yana haki; hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi.” Naam, mafundisho ya hekima ni bora kabisa na ya unyofu, ni ya kweli na ya uadilifu. Hayana udanganyifu au upotovu wowote. “Yote humwelea yule afahamuye, yote huelekea mbele yao waliopata maarifa.”—Mithali 8:6-9.
Kwa kufaa, hekima yahimiza hivi: “Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, na maarifa kuliko dhahabu safi.” Ombi hilo ni la busara, “maana hekima ni bora kuliko marijani; wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.” (Mithali 8:10, 11) Lakini ni kwa nini? Ni nini hufanya hekima iwe yenye thamani kuliko mali?
“Matunda Yangu Hupita Dhahabu”
Zawadi wanazopata wale wanaoisikiliza hekima ni zenye thamani zaidi ya dhahabu, fedha, au marijani. Ikifafanua zawadi hizo, hekima yasema hivi: “Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu; natafuta maarifa na busara. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; kiburi na majivuno, na njia mbovu, na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.”—Mithali 8:12, 13.
Hekima humpa yule aliye nayo werevu na maarifa. Mtu mwenye hekima ya kimungu ana staha na kicho pia kuelekea Mungu, kwa kuwa “kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima.” (Mithali 9:10) Kwa hiyo, anachukia kile Yehova anachochukia. Hana kiburi, wala majivuno, wala njia mbovu, wala kinywa cha ukaidi. Kuchukia lililo ovu humzuia asitumie mamlaka kwa njia ya kibinafsi. Ni jambo la maana kama nini kwamba wale wenye madaraka katika kutaniko la Kikristo, pamoja na vichwa vya familia, watafute hekima!
“Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi,” hekima yaendelea kusema. “Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu. Kwa msaada wangu wafalme humiliki, na wakuu wanahukumu haki. Kwa msaada wangu wakuu hutawala, na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia.” (Mithali 8:14-16) Matunda ya hekima yatia ndani ufahamu wenye kina, uelewevu, na nguvu—sifa zinazohitajiwa sana na watawala, maofisa wa cheo cha juu, na wakuu. Hekima ni muhimu kwa wale walio na mamlaka na wale wanaowashauri wengine.
Hekima ya kweli hupatikana kwa wote kwa urahisi lakini si wote wanaoipata. Wengine huikataa au kuikwepa, hata wakati wanapoweza kuipata kwa urahisi. “Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona,” yasema hekima. (Mithali 8:17) Hekima hupatikana tu kwa wale wanaoitafuta kwa bidii.
Njia za hekima ni za unyofu na uadilifu. Huwanufaisha wale wanaoitafuta. Hekima husema:“Utajiri na heshima ziko kwangu, naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao.”—Mithali 8:18-21.
Zawadi za hekima zatia ndani sifa bora kabisa kama vile busara, uwezo wa kufikiri, unyenyekevu, ufahamu wenye kina, hekima itumikayo, na uelewevu, na vilevile mali na heshima. Mtu mwenye hekima anaweza kupata mali kwa njia ya uadilifu, na atasitawi kiroho. (3 Yohana 2) Hekima humfanya mtu aheshimike pia. Isitoshe, anaridhika na kile anachopata, na ana amani ya akili na dhamiri safi mbele za Mungu. Naam, heri mtu yule aonaye hekima. Kwa kweli matunda ya hekima ni bora kuliko dhahabu safi na fedha iliyo teule.
Shauri hilo ni la wakati unaofaa kama nini kwetu, kwa kuwa tunaishi katika ulimwengu unaofuatia vitu vya kimwili na ambao hukazia kupata mali kwa njia yoyote ile! Na tusisahau kamwe thamani ya hekima wala tusitumie njia zisizo za haki kujipatia mali. Na tusipuuze kamwe maandalizi hasa yanayotoa hekima—mikutano yetu ya Kikristo na funzo la kibinafsi la Biblia na vichapo vinavyoandaliwa na “mtumwa mwaminifu na mwenye busara”—kwa ajili tu ya kujipatia mali.—Mathayo 24:45-47.
“Nalitukuka Tokea Milele”
Katika sura ya 8 ya Mithali hekima haifananishwi na mtu ili kufafanua sifa fulani ya kuwazia tu. Kwa njia ya ufananisho, hekima yarejezea pia uumbaji wa Yehova ulio wa maana zaidi. Hekima yaendelea kusema: “BWANA alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake, kabla ya matendo yake ya kale. Nalitukuka tokea milele, tangu awali, kabla haijawako dunia. Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa, wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji. Kabla milima haijawekwa imara, kabla ya vilima nalizaliwa. Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde wala chanzo cha mavumbi ya dunia.”—Mithali 8:22-26.
Ufafanuzi uliotangulia wa hekima inayofananishwa na mtu walingana kama nini na yale yanayosemwa na Maandiko kuhusu “Neno”! “Hapo mwanzoni Neno alikuwako, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa mungu,” akaandika mtume Yohana. (Yohana 1:1) Hekima inayofananishwa na mtu yawakilisha kwa njia ya mfano Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, kabla ya kuwa mwanadamu.*
Yesu Kristo ni “mzaliwa wa kwanza wa uumbaji wote; kwa sababu kwa njia yake vitu vingine vyote viliumbwa katika mbingu na juu ya dunia, vitu vinavyoonekana na vitu visivyoonekana.” (Wakolosai 1:15, 16) Hekima inayofananishwa na mtu yaendelea kusema: “[Yehova]alipozithibitisha mbingu nalikuwako; alipopiga duara katika uso wa bahari; alipofanya imara mawingu yaliyo juu; chemchemi za bahari zilipopata nguvu; alipoipa bahari mpaka wake, kwamba maji yake yasiasi amri yake; alipoiagiza misingi ya nchi; ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; nikawa furaha yake kila siku; nikifurahi daima mbele zake; nikiifurahia dunia inayokaliwa na watu; na furaha yangu ilikuwa pamoja na wanadamu.”(Mithali 8:27-31) Mwana mzaliwa wa kwanza wa Yehova alikuwa kando ya Baba yake, akifanya kazi kwa bidii pamoja naye—Muumba asiye na kifani wa mbingu na dunia. Yehova Mungu alipoumba mwanadamu wa kwanza, Mwana Wake alishiriki kazi hiyo akiwa Stadi wa Kazi. (Mwanzo 1:26) Si ajabu kwamba Mwana wa Mungu anawapenda sana wanadamu!
“Ana Heri Mtu Yule Anisikilizaye”
Akiwa kama hekima inayofananishwa na mtu, Mwana wa Mungu asema: “Basi, wanangu, nisikilizeni sasa; maana heri hao wazishikao amri zangu. Sikieni mafundisho, mpate hekima, wala msiikatae. Ana heri mtu yule anisikilizaye, akisubiri sikuzote malangoni pangu, akingoja penye vizingiti vya milango yangu. Maana yeye anionaye mimi aona uzima, naye atapata kibali kwa BWANA. Bali anikosaye hujidhuru nafsi yake mwenyewe, na wao wanichukiao hupenda mauti.”—Mithali 8:32-36.
Yesu Kristo ndiye mfano halisi wa hekima ya Mungu. “Zenye kusitiriwa kwa uangalifu ndani yake ni hazina zote za hekima na za ujuzi.” (Wakolosai 2:3) Acheni basi, tumsikilize kwa makini na kufuata hatua zake kwa ukaribu. (1 Petro 2:21) Kumkataa ni kuangamiza nafsi yetu wenyewe na kupenda kifo, kwa kuwa “hakuna wokovu katika mwingine yeyote.” (Matendo 4:12) Kwa kweli, acheni tumkubali Yesu kuwa mtu ambaye Mungu ametoa kwa ajili ya wokovu wetu. (Mathayo 20:28; Yohana 3:16) Kwa kufanya hivyo tutapata furaha inayotokana na ‘kuona uzima na kupata kibali kwa Yehova.’
[Maelezo ya Chini]
Neno la Kiebrania lililotafsiriwa “hekima” liko katika ngeli ya kike. Kwa hiyo, watafsiri fulani hutumia viwakilishi vya ngeli ya kike wanaporejezea hekima.
Uhakika wa kwamba neno la Kiebrania “hekima” sikuzote huwa katika ngeli ya kike haupingani na matumizi ya hekima kuwakilisha Mwana wa Mungu. Neno la Kigiriki “upendo” katika usemi “Mungu ni upendo” liko katika ngeli ya kike pia. (1 Yohana 4:8) Hata hivyo, linatumiwa kurejezea Mungu.
[Picha katika ukurasa wa 26]
Hekima ni muhimu sana kwa wale walio na madaraka
[Picha katika ukurasa wa 27]
Usipuuze maandalizi yanayotoa hekima
Read more »

Wednesday, January 27, 2016

Jifunze namna ya kupunguza Uzito

Jinsi ya Kupunguza Uzito (2)
Assalaamu Alaykum wasikilizaji wapenzi wa kipindi cha afya. Nina wingi wa matumaini kuwa mu bukheri wa afya mkiitegea sikio Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kama mtakumbuka wiki iliyopita tulianza kuzungumzia jinsi ya kupunguza uzito wa kupindukia na tumbo, ambapo tulielezea mpango maalumu wa lishe na mazoezi wa kufuatwa ili kufanikisha suala hilo au diet plan. Leo hii pamoja na mambo mengine tutaendelea kuelezea mpango huo kwa ajili ya siku ya pili na ya tatu na tumeahidi kuendelea kuwabainishia mpango huo unaofaa kutumiwa kwa muda wa siku 7 ili kujibu maombi ya wasikilizaji wetu.  Tafadhalini msiondoke kando ya redio zenu hadi mwisho wa kipindi.

&&&&&&
Katika siku ya pili:
Unapaswa kutembea kwa nusu saa asubuhi na kufanya sit-ups 15-30. Baada ya mazoezi kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kunywa kikombe kimoja cha chai au kahawa kwa kuweka kijiko kimoja cha sukari kidogo kama nilivyoeleza huko nyuma katika siku ya kwanza.Unaweza kulasausage moja ya kuchemsha ya kuku au ya nyama ya ngombe. Kipande kimoja cha mkate uliotengenezwa kwa ngano isiyokobolewa au brown breadpamoja na matunda kwa kiasi utakacho.Chakula cha  mchana (lunch): Kula ndizi moja ya kuchoma pamoja na kachumbari au saladiya mboga aina yoyote lakini isiwe na mayonnaise. Kula mishikaki miwili au mitatu ya nyama ya ngombe (isiwe ya nundu au nyama ya mafuta), kuku au samaki.Jioni:Tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa (dakika 30) na baada ya hapo fanya sit-ups 15-20 kisha kunywa maji ya uvuguvugu bilauri 


Read more »

Wednesday, January 13, 2016

Huu Ndio Mwonekano wa Hekalu la Mfalme Suleimani, Jerusalemu kama Inavyotajwa kwenye Biblia





Lakini pamoja na Picha hizi pia nimekuwekea na Somo kama lilivyoandikwa na Charles Mwaisemba

MFULULIZO WA MASOMO YA MATUKIO YA MWISHO WA DUNIA 
SOMO 3:DHIKI KUBWA (PART 4) 
4) NJIA YA KUPATA WOKOVU WAKATI WA DHIKI KUU Kwa wayahudi kwao Wokovu wao unapatikana kwa njia mbili maana Mungu alikuwa amekwishajifunga kwenye Neno lake Kuwa atawaokoa Biblia inasema katika WARUMI 11:25-31,
 I. Ni kutokumsujudia mnyama au sanamu yake, na kutokupokea chapa ya '666' ambayo itawapelekea wakubali kuteswa hata ikibi kufa ndipo wataokolewa 
II. Kukimbilia mahali maarufu palipowekwa na Mungu mwenyewe,Biblia ndio inapataja kama milimani lakini ndio hii sehemu inayojulikana kama PETRA katika Mlima ule wa Mizeituni,mahali pale ambapo Yesu alipaa kwenda mbinguni na ndipo atakaporudi mara ya pili,nao wote waliokimbilia milimani ndipo watakapomuombolezea Yeye waliyemchoma na waliomkataa Mwanzo
Endelea kusoma zaidi hapa>>BOFYA HAPA

Read more »

Tuesday, January 12, 2016

The Story of Hebron (Historia Ya Hebroni)

Hebron City
The foundation of this important and ancient city of Palestine is mentioned in the Old Testament in a unique manner: "And Hebron was built seven years before Zoan of Egypt" (Nu. 13:22). The date of the foundation of Zoan, which served as the capital of the Hyksos, can be calculated from extra-biblical sources as circa 1720 BC. It may therefore be assumed that Hebron was built at the beginning of the Middle Bronze (Canaanite) Age 11, which coincides with the Hyksos period. This estimate is also borne out by the frequent mention of Hebron in the Patriarchal Epics (Genesis 13:18; 35:27, and elsewhere), as the Patriarchal period also coincides with that of the Hyksos.
King David and Hebron (extra information)
The Second Book of Samuel opens with David's lament over Saul and Jonathan and David's move to Hebron, the tribal and cultic centre of Judah and close to Bethlehem, David's birthplace.
At Hebron, David was anointed king over Judah (II Sam. 2:4). In the interim, Saul's commander Abner had crowned Saul's son Ishbaal (Ishbosheth) king of northern Israel at Mahanaim (II K. 2:8-10). After Saul's defeat and death, the Philistines appear to have recognized two separate vassal kingdoms in western Palestine: the area which David ruled from Hebron and the northern territory which acknowledged Ishbaal (2:9). After some desultory fighting, David defeated Ishbaal, apparently without any intervention by the Philistines. With Ishbaal dead, the northern tribes of Israel accepted David's leadership and, by the eighth year of his reign, he felt himself strong enough to make a bid for independence and the unity of his kingdom.

Read more »
 

Followers


LinkWithin

Hebroni 2016. Powered by Blogger.