BONYEZA PICHA HILI CHINI UWE MIONGONI MWA WANAONUFAIKA NA...☟⇓
Assalaamu Alaykum wasikilizaji wapenzi wa kipindi cha afya. Nina wingi wa matumaini kuwa mu bukheri wa afya mkiitegea sikio Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kama mtakumbuka wiki iliyopita tulianza kuzungumzia jinsi ya kupunguza uzito wa kupindukia na tumbo, ambapo tulielezea mpango maalumu wa lishe na mazoezi wa kufuatwa ili kufanikisha suala hilo au diet plan. Leo hii pamoja na mambo mengine tutaendelea kuelezea mpango huo kwa ajili ya siku ya pili na ya tatu na tumeahidi kuendelea kuwabainishia mpango huo unaofaa kutumiwa kwa muda wa siku 7 ili kujibu maombi ya wasikilizaji wetu. Tafadhalini msiondoke kando ya redio zenu hadi mwisho wa kipindi.
&&&&&&
Katika siku ya pili:
Unapaswa kutembea kwa nusu saa asubuhi na kufanya sit-ups 15-30. Baada ya mazoezi kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kunywa kikombe kimoja cha chai au kahawa kwa kuweka kijiko kimoja cha sukari kidogo kama nilivyoeleza huko nyuma katika siku ya kwanza.Unaweza kulasausage moja ya kuchemsha ya kuku au ya nyama ya ngombe. Kipande kimoja cha mkate uliotengenezwa kwa ngano isiyokobolewa au brown breadpamoja na matunda kwa kiasi utakacho.Chakula cha mchana (lunch): Kula ndizi moja ya kuchoma pamoja na kachumbari au saladiya mboga aina yoyote lakini isiwe na mayonnaise. Kula mishikaki miwili au mitatu ya nyama ya ngombe (isiwe ya nundu au nyama ya mafuta), kuku au samaki.Jioni:Tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa (dakika 30) na baada ya hapo fanya sit-ups 15-20 kisha kunywa maji ya uvuguvugu bilauri
4. Epuka juisi aina yoyote ile iwe freshi au za kwenye boksi kwani mara nyingi watu huhadaiwa na juisi za kwenye maboksi zinazoandikwa kuwa ni freshi na zisizo na kemikali yoyote. Baadhi ya wakati kampuni zinazotengeneza juisi hizi huzipa tenda kampuni za kutengeneza manukato ambazo ndizo hutengeneza maboksi haya na kuweka syrup na harufu kulingana na harufu ya tunda linalohitajika. Kwa mfano kama kampuni ya kutengeneza juisi inahitaji boksi la harufu ya embe basi watawatengenezea boksi hilo kwa kutumia syrup ya embe na harufu ya embe. Pia juisi za kwenye maboksi, wakati wa kutengenezwa huhifadhiwa kwa muda mrefu na kupitia mlolongo mrefu wa utengenezaji hivyo kuondoa virutubisho asilia muhimu kwa ajili ya mwili pamoja na ufumwele ambazo ni muhimu sana kiafya.Chakula cha usiku (dinner): KunywaSupu ya mboga mboga (vegetable soup) pamoja na matunda. Epuka ndizi mbivu. Epuka vileo vya aina yoyote sigara, tumbaku, na kadhalika.
4. Epuka juisi aina yoyote ile iwe freshi au za kwenye boksi kwani mara nyingi watu huhadaiwa na juisi za kwenye maboksi zinazoandikwa kuwa ni freshi na zisizo na kemikali yoyote. Baadhi ya wakati kampuni zinazotengeneza juisi hizi huzipa tenda kampuni za kutengeneza manukato ambazo ndizo hutengeneza maboksi haya na kuweka syrup na harufu kulingana na harufu ya tunda linalohitajika. Kwa mfano kama kampuni ya kutengeneza juisi inahitaji boksi la harufu ya embe basi watawatengenezea boksi hilo kwa kutumia syrup ya embe na harufu ya embe. Pia juisi za kwenye maboksi, wakati wa kutengenezwa huhifadhiwa kwa muda mrefu na kupitia mlolongo mrefu wa utengenezaji hivyo kuondoa virutubisho asilia muhimu kwa ajili ya mwili pamoja na ufumwele ambazo ni muhimu sana kiafya.Chakula cha usiku (dinner): KunywaSupu ya mboga mboga (vegetable soup) pamoja na matunda. Epuka ndizi mbivu. Epuka vileo vya aina yoyote sigara, tumbaku, na kadhalika.
Siku ya Tatu:
Fanyamazoezi kama kawaida. Kimbia au tembea kwa dakika 30, kisha fanyasit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.Mlo wa asubuhi (breakfast): Kunywa kikombe kimoja cha chai au kahawa kikiwa na kijiko kimoja kidogo cha sukari.Chakula cha mchana (lunch):Kunywa maji ya uvuguvugu bilauri 4 kabla au baada ya kula. Kula ndizi mbili za kuchemsha (maarufu kama ndizi Bukoba) na siyo ndizi tamu. Kula piabakuli la kutosha la supu ya mboga mboga ukishushia kwa matunda kwa wingi. Epuka ndizi mbivu. Hakikisha wakati wa kupika supu yako huweki mafuta ya kupikia, siagi na kadhalika.Jioni:Tembea au kimbia kwa muda wa nusu saa. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 baada ya kufanya mazoezi. Unaweza kula matunda wakati unasubiria chakula cha usiku.Chakula cha Usiku (dinner):Oka sausage 3 au kipande cha nyama pamoja na saladi au kachumbari.
&&&&&&
Wasikilizaji wapenzi tunasonga mbele na kipindi chetu ambapo baada ya kuelezea diet plan ya siku ya pili na ya tatu, hebu sasa tuzungumzie umuhimu wa kufanya mazoezi na wakati bora wa kufanya mazoezi hayo. Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kupunguza mafuta ya ziada mwilini. Tafiti zinaonesha kuwa mtu asiyefanya mazoezi hupata madhara makubwa ya kiafya.
Tutupie jicho utafiti unaotujuza kuwa, kufanya mazoezi kabla ya kufungua kinywa hupunguza mafuta mwilini. Kwa mujibu wa utafiti huo, daktari mmoja aitwaye Mackod, alipitia makala nyingi za afya ili kuweza kutambua visababishi vya vifo visivyotokana na umri au nasaba ya kiasili (genetic), na akagundua mambo tisa yanayosabisha vifo ambavyo vingeweza kuzuilika. Mambo hayo tisa ni uvutaji sigara, unywaji pombe, kutofanya mazoezi, lishe duni, wadudu kama bakteria na virusi, ajali, tabia za kufanya ngono kupita kiasi bila kinga, vita na madawa ya kulevya. Utafiti huo uliofanywa na Dr. Jason na Nor Farah wa Chuo kikuu cha Glasgow, umeonesha kuwa kufanya mazoezi kabla ya kifungua kinywa, wakati tumbo likiwa tupu, ni bora zaidi kuliko kufanya mazoezi baada ya mlo wowote. Kufanya mazoezi ni jambo la maana kwa afya kuliko kutofanya mazoezi ya mwili, lakini unaweza kupata faida zaidi kama unaweza kufanya mazoezi hayo kabla hujala chochote.
Mazoezi kwa ujumla yana umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu, hasa kama yataambatana na lishe bora. Mazoezi huweza kuzuia magonjwa sugu kama vile kisukari, magonjwa ya moyo, kensa na shinikizo la damu, na pia kwa kufanya mazoezi unaweza kuongeza kipato kwa kuwa unaweza kufanya kazi muda mrefu kuliko asiyefanya mazoezi kutokana na kuwa na siha njema. Familia ambazo hufanya mazoezi huwa na afya bora huku kipato wanachokipata kikitumika kwenye maendeleo ambapo familia zisizofanya mazoezi, hujikuta zikitumia kipato hicho kwa ajili ya kutibu magonjwa ambayo yangeepukika kwa kufanya mazoezi.
Pia kufanya mazoezi kila mara na hasa kabla ya mlo kuna faida nyingi ambazo haziwezi kuonekana kwa haraka, kama vile kuimarisha akili, ambayo matokeo yake ni kuwa na furaha. Hii inatokana na kuzalishwa kwa wingi kemikali aina ya endorphins wakati wa kufanya mazoezi. Kemikali hii ni muhimu katika kupambana na msononeko wa mawazo (depression) na hivyo humfanya mtu anayefanya mazoezi awe na furaha zaidi. Tafiti zinaonesha kuwa, mwili huzalisha kemikali hii ya endorphins baada ya mtu kufanya mazoezi ya kawaida kwa dakika 12. Kama wanafamilia wanaweza kufanya mazoezi kwa muda hata wa saa moja, au nusu saa, wanaweza kuwa na furaha na pengine kuzuia misononeko katika familia na hata kusambaratika ndoa.
&&&&&&&&
Pia kuna kemikali nyingine muhimu ambayo tafiti zinaonesha kuwa huzalishwa baada ya kufanya mazoezi. Kemikali hii iitwayo "serotonin" huongezeka kwenye mfumo wa neva baada ya kufanya mazoezi, na humfanya mfanya mazoezi ajisikie vizuri kiafya na kupunguza msongo wa mawazo pia. Chunguzi pia zinabainisha kuwa kemikali hii, ni muhimu sana katika mwili, kwani hufanya mfanya mazoezi alale usingizi mnono.
Ufanyaji wa mazoezi mara kwa mara husaidia pia mfanya mazoezi ajithamini, na kuondoa uchovu na unyonge. Faida nyingine ya kufanya mazoezi tunaelezwa kuwa ni kufanya tendo la ndoa kuwa bora na hivyo kuleta mahusiano mazuri ya kinyumba. Kwa ujumla wapenzi wasikilizaji utafiti huo unaainisha umuhimu na faida za mazoezi na matokeo yake ili kuleta hamasa ya kufanya mazoezi kwa kila mtu. Unaweza kufanya mazoezi wewe na familia yako, na wenzako, au pekee yako. Chukua muda kidogo katika masaa 24 na jitahidi kufanya mazoezi, ili ujisikie vizuri na kuwa mwenye siha. Lakini kumbuka kuwa, tunapata faida zaidi tukifanya mazoezi wakati tumbo likiwa tupu, yaani kabla ya mlo, baada ya kula chakula tunashauriwa ni bora tutetembee taratibu ili kukifanya chakula kitulie vyema tumboni. Faida nyingine ya kufanya mazoezi asubuhi kabla ya kula chochote ni kuongeza umetaboli au kitendo cha ujenzi wa seli na uvunjaji vunjaji wa kemikali zinazotokana na chakula mwilini, kwa kimombo 'metabolism', suala linalosaidia sana kupunguza unene. Hii ni kwa sababu watu wengi wanapofikia umri wa miaka 35 na kuendelea, kiwango cha umetaboli hupungua na hivyo kuwa wanene. Hivyo ni bora, tujitahidi kufanya mazoezi angalau kwa muda wa robo saa kwa siku, wakati wa asubuhi kabla ya kifungua kinywa.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.
Jiunge Nasi Tuwe Tunakutumia Habari Mara tu zinapotokea! ..Bofya HAPA Ujiunge Sasa..
BONYEZA PICHA HILI CHINI UWE MIONGONI MWA WANAONUFAIKA NA...☟⇓
0 comments:
POST A COMMENT