Hebroni: Matukio
Habari Mpya
Loading...
Showing posts with label Matukio. Show all posts
Showing posts with label Matukio. Show all posts

Tuesday, June 14, 2016

MKUU WA WILAYA YA IRINGA ASHIRIKI MAZISHI YA MAMA MKWE WA Mch. HUNTER MURO

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alishiriki katika mazishi ya Mama Mkwe wa Mkuu wa jimbo la Kaskazini Dayosisi ya Mashariki na Pwani(DSM) Mch Hunter Muro, Mama Emiliana Magava ambaye pia ni Mama Mdogo wa wabunge Mh.Venance Mwamoto na Mh.Rita Kabati. Mazishi hayo yalifanyika wilaya ya Kilolo Iringa. Akiwafariji wafiwa Mh Kasesela alisema " Kuna aina mbili ya vifo hapa duniani vipo vifo kwa mapenzi ya Mungu kama Mama yetu Emiliana lakini pia vipo vifo vya kujitakia ambavyo tunamsingizia Mungu eti mapenzi yake" Aliendela kwa kuvitaja vifo kama kuendesha bodabdoa ovyo na kwa mbwembwe bila kuvaa kofia, kuendesha gari umelewa na vingine vingi vinavyo fanana. Katika kutoa shukrani Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo ambaye pia alikuwa msemaji wa familia alisema imefika wakati wachungaji waruhusiwe kuchapa viboko kwani waumini wamekuwa na kiburi sana.​

Read more »

Tuesday, May 10, 2016

VIJANA WA IRINGA Mpo? Ni Zamu Yenu sasa

Usisite Kutujulisha ili tutangaze huduma ya Mungu kupitia anwani yetu
donatusdk@gmail.com

Read more »

Sunday, January 17, 2016

PICHAZ: Tamasha La Uimbaji Lililofanyika K.K.K.T Kimara; Kwaya Mbalimbali Zilikuwepo km; Uinjiliji Kijitonyama, Uinjilisti Kimara.

Waimbaji wakiabudu tayari kufungua tamasha

Waimbaji wakiabudu tayari kuanza tamasha

Read more »

Wednesday, January 13, 2016

Kutoka Viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza; Katika Maombi ya Kumwombea Rais Magufuli


Januari 13,2016 Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza unawakutanisha Watanzania katika Uwanja wa Furahisha uliopo katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa ajili ya Maombi ya rasmi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wasaidizi wake ili kuliongoza Taifa vema. Pia maombi hayo ni mahususi kwa ajili ya kuliombea Taifa kwa ajili ya kupata baraka mbalimbali. Kuanzia majira ya saa saba Wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wameanza kujongea kwa ajili ya kujumuika pamoja katika maombi hayo ambayo yatafikia tamati jioni. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo huku wageni mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini pamoja na waimbaji nyimbo za injili wakihudhuria katika maombi hayo
Credit>Rumaafrica
Read more »

Tuesday, January 12, 2016

Maandalizi ya Campus Night ARUSHA Yazidi kukamilika; Itafnyika Ijumaa Hii.... Tar 15/1/2016

Zikiwa zimebakia siku mbili kulekea mkesha wa Campus Night 2016 pale SheikAmri Abeid Karume jijini Arusha ambalo limeandaliwa na Manna Tabernacle Bible Church (MTBC) - Moshi tarehe 15 januari mwaka huu kuanzia saa mbili usiku,tayari jukwaa limeshaanza kufungwa katika katika huo.


fb/John Pazia

fb/John Pazia

Tukio hilo itahusisha waimbaji mbali mbali wa muziki wa injili kama Angel Benard,Paul Clement, MTBC Praise Team,VOT,Abenego & The Worshipers na wengine wengi,Ambapowahudumu wakiwa ni Mchungaji Dickson Mtalitinya(mwenyeji) pamoja na Martin & Jannekah Gooya(nairobi).
Chanzo: Gospel Kitaa
Read more »
 

Followers


LinkWithin

Hebroni 2016. Powered by Blogger.