Hebroni
Habari Mpya
Loading...

Tuesday, June 14, 2016

MKUU WA WILAYA YA IRINGA ASHIRIKI MAZISHI YA MAMA MKWE WA Mch. HUNTER MURO

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alishiriki katika mazishi ya Mama Mkwe wa Mkuu wa jimbo la Kaskazini Dayosisi ya Mashariki na Pwani(DSM) Mch Hunter Muro, Mama Emiliana Magava ambaye pia ni Mama Mdogo wa wabunge Mh.Venance Mwamoto na Mh.Rita Kabati. Mazishi hayo yalifanyika wilaya ya Kilolo Iringa. Akiwafariji wafiwa Mh Kasesela alisema " Kuna aina mbili ya vifo hapa duniani vipo vifo kwa mapenzi ya Mungu kama Mama yetu Emiliana lakini pia vipo vifo vya kujitakia ambavyo tunamsingizia Mungu eti mapenzi yake" Aliendela kwa kuvitaja vifo kama kuendesha bodabdoa ovyo na kwa mbwembwe bila kuvaa kofia, kuendesha gari umelewa na vingine vingi vinavyo fanana. Katika kutoa shukrani Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo ambaye pia alikuwa msemaji wa familia alisema imefika wakati wachungaji waruhusiwe kuchapa viboko kwani waumini wamekuwa na kiburi sana.​

Read more »

Tuesday, May 10, 2016

ZIJUE BARAKA ZA KUJITOA

Wanafunzi wa kwanza wa Yesu wakaacha yote wakamfuata. Wengine waliacha nyavu zao, na wengine wakaacha shughuli zingine. Wengine waliacha familia zao kwa muda mrefu ili wahubiri injili. Wakristo wengi katika historia wamejitoa bila kuangalia faida zao wenyewe ili injili iwafikie watu wengine, na hivyo wamefanyika baraka kwa mataifa. Bila watu kujitoa ukristo ungekuwa umekufa zamani. Mtu anaweza kutoa mali, muda, kazi n.k. katika ufalme wa Mungu, lakini Biblia inatuonyesha kwamba hayo yote yanaanza kwa kujitoa mwenyewe, yaani moyo. Bila kujitoa mwenyewe hayo yote mengine hayana maana mbele za Mungu. (Mika 6:6-8)

Mtajiri na maskini anaweza kujitoa:

2 Kor 8:1-5 
Baadhi ya makanisa yalikuwa yameamua kuwasaidia wakristo wa Yerusalemu waliopatwa na shida ya njaa. Paulo anawaandikia Wakorintho akiwataja Wamakedonia kama mfano mzuri wa kujitoa. Wamakedonia walikuwa hawana mali nyingi. Wenyewe waliishi kwa shida. Hata hivyo walitoa hata kupita uwezo wao ili wasaidie wenzao huko Yerusalemu. Paulo anasema walijitoa nafsi zao kwanza kwa Bwana, na hata kwa ndugu zao katika imani.
2 Kor 8:7
Wakorintho ambao walikuwa hawakosi kitu waliambiwa watoe kwa ukarimu. Wajitoe wenyewe kama Wamakedonia walivofanya.

Yesu ni mfano mkuu wa kujitoa:

Rum 15:3 
2 Kor 8:9 
Fil 2:4-8 
Yn 3:16 
Kujitoa inamaanisha kujali mahitaji ya wengine. Usifikirie mahitji yako mwenyewe tu. Huenda mwenzako ana mahitaji makubwa kuliko wewe. Jirani yako huenda anapotea katika dhambi wakati wewe unatafuta mali ya dunia hii. Yesu alikuwa ana kila kitu alipoishi mbinguni, lakini akaamua kuzaliwa horini kama mtu maskini, na akafa msalabani ili sisi tusipotee.


Kwa nini tujitoe?

Fil 2:9-12
Kwa ajili ya kujitoa kwake Yesu Mungu akamwinua juu ya yote. Kwa nini Mungu akafanya hivyo?
Yn 12:24
Sheria ya kiroho inasema; Ili uhai upatikane, lazima kifo kiwepo kwanza. Unapojitoa kwa Mungu maisha yatakuwa yenye maana zaidi. Usipojitoa na moyo wako wote huenda utapotea, au utaokoka kwa neema, lakini utabaki kama mbegu pekee isiopandwa ardhini. Mbegu ikipandwa ardhini inazaa. Unapojitoa mia kwa mia unapandwa kama mbegu ardhini. Kwa namna fulani unakufa, lakini utazaa matunda. Mimi binafsi ninaomba nikifika mbele za Mungu siku moja nije pamoja na watu waliomwamini kwa sababu ya kujitoa kwangu.


Faida za kujitoa:

2 Kor 9:6-8

Faida ya kwanza: Mahitaji yako ya kila siku utayapata

Anayetoa mali, muda wake, nguvu zake na moyo wake wote kwa furaha na kwa hiari yake mwenyewe ameahidiwa kwamba mahitaji yake ya kila siku atayapata. Na Mungu anajaza kikombe chake mpaka kinafurika. Anapewa uwezo wa kutoa tena, na ngurudumu ya baraka kwake na kwa wengine inaanza kuzunguka.
2 Kor 9:13-14

Faida ya pili: Watu watakuombea.

Ukijitoa kwelikweli kwa Bwana utakuta watu wengine wanabarikiwa. Haitakuwa vigumu kwao kukukumbuka wanapomwomba Mungu. Mtu anayeombewa na wenzake anapata ushindi hata anapopita katika magumu maishani.

Faida ya tatu: Jina la Bwana litasifiwa.

Mkristo alieokoka ana lengo moja tu: kumtumikia Mungu. Mtu anapojitoa jina la Bwana linasifiwa. Ufalme wa Mungu unaenea. Mkristo wa kweli ataona hii ni faida kubwa sana.
Read more »

VIJANA WA IRINGA Mpo? Ni Zamu Yenu sasa

Usisite Kutujulisha ili tutangaze huduma ya Mungu kupitia anwani yetu
donatusdk@gmail.com

Read more »

Sunday, May 8, 2016

Dalili za Mtumishi wa Mungu kwelikweli

– Mtumishi wa Mungu hawatawali washirika wa kanisa.
“Yesu akawaita, akawaambia, ‘Wafalme wa Mataifa huwatawala,…na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini kwenu ninyi sivyo; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu, na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote.” (Luka 22:25; Marko 10:42-44).
Mtumishi wa kweli hajifanyi kama ‘Bwana’ juu ya watu wa Mungu – hajiinui juu ya washirika kama ‘rais’ wa watu. Kumbuka, Bwana Yesu, Mwana wa Mungu, alisema ‘KWENU NINYI SIVYO’. Mchungaji huharibu sura ya Yesu machoni pa watu kama akitawala kama ‘mkuu wa kijiji’ juu ya washirika; ameacha tabia ya Yesu kama anajifanya ‘mkubwa’ kanisani. Hayo yote ni kosa kubwa sana. Kama mchungaji akiwatawala watu kwa nguvu, ndipo yeye hafuati Yesu. Paulo aliandika juu ya huduma yake, “Si kwamba tunatawala imani yenu; bali tu WASAIDIZI wa furaha yenu… Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu WATUMISHI WENU kwa ajili ya Yesu.” (2 Wakor.1:24; 4:5).
Mtume Petro aliwaandikia wazee/wachungaji ifuatyo: “lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. WALA SI KAMA WAJIFANYAO MABWANA JUU YA MITAA YAO, bali kwa kujifanya VIELELEZO kwa lile kundi.” (Waebr.13:2,3). Inapaswa mtumishi wa Mungu awe kielelezo kwa washirika na siyo kujifanya ‘Bwana’. Bwana Yesu ametufundisha inapaswa awe ‘mtumishi’ au ‘mtumwa’ wa washirika!
– Kwa sababu ya upendo wake kwa kunid la Bwana, mtumishi wa Mungu yupo tayari kutoa maisha yake kwa ajili ya kundi la Bwana hata kama Yesu Kristo alivyofanya, “nasi tukiwatumaini KWA UPENDO MWINGI, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, BALI NA ROHO ZETU pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.” (1 Wathes.2:8). Kwa hiyo…
– Mtumishi wa Mungu kwelikweli anawatumikia washirika kwa upole and unyenyekevu:
“bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe… mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu nikiwapo pamoja nanyi” (1 Wathes.2:7; 2 Wakor.10:1).
– Kwa maneno na matendo yake mtumishi wa kweli hachukizi dhamiri za washirika – dhamiri zao zinamshuhudia kwamba mwendo wake ni safi kabisa katika sehemu yote!
“tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, DHAMIRI ZA WATU ZIKITUSHUHUDIA MBELE ZA MUNGU…Ninyi ni mashahidi, na MUNGU PIA, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;  (2 Wakor.4:2; 1 Wathes.2:10). 
Hakuna sababu kumlaumu! “Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe.” (2 Wakor.6:3). Na hata Mungu ni shahidi mwendo wake! (1 Wathes.2:5).
– Mtumishi wa kweli wa Mungu HATAFUTI fedha zako. HATAMANI pesa zako wala hatakulazimisha umpe pesa kwa ajili ya huduma au maombi yake.
“Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.” (Matendo 20:33). Huyu ni mtumishi wa Mungu kwelikweli.
– Mtumishi wa Mungu HATAFUTI kujifanya mtajiri kupitia huduma yake kwako.
“Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho.” (Mat.3:6). Mtume Petro pamoja na mitume wengine walipokea pesa nyingi sana kwa ajili ya waumini maskini lakini, kumbe, hawakuchukua pesa kwa ajili ya faida yao kujifanya matajiri! Hawakuishi kwenye nyumba ya fahari wala hawakuwa na walinzi wa binafsi. (Au unafakiri Petro au Paulo wangeweza kuwa na magari mengi ya gharama kubwa sana au kuishi katika nyumba ya fahari au kuwa na ndege ya binafsi kama ‘wahubiri’ wengine siku hizi? Je, unafikiri kuishi kwa fahari kama hiyo inawakilisha tabia ya Yesu Kristo?) Mitume wa Bwana walikuwa na moyo safi na walifanya huduma yao bila unyonyaji, “Maana hatukuwa na … maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.” (1 Wathes.2:5). “Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila gharama, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili.” (1 Wakor.9:18).
Neno la Mungu ni dhidi wachungaji ambao wanawahudumia watu Wake kwa ajili ya faida zao, kujitajirisha wenyewe. “Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo? …Mnawala walionona, mnajivika manyoya, …lakini hamwalishi kondoo.” Ezekieli 34:2,3.
– Mtumishi wa Mungu HATAFUTI vyake mwenyewe.
“Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu.” Tutambue, Paulo anasema ‘wote’! Basi, kwa uhakika maana yake ni idadi isiyopungua ‘wengi’! Ina maana, watumishi wengi/wote (ila Timotheo) walitafuta vyao wenyewe! Walitumia huduma yao kwa ajili ya faida yao yenyewe. Jambo la kuhuzunishwa sana! Je, ni tofauti sana siku hizi?
– Mtumishi wa Mungu HATAFUTI kuwapendeza watu, hasemi mambo kwa kusudi la kuvuta watu kanisani kwake ili ajenge kanisa kubwa kwa ajili ya sifa yake.
“Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.” (Wagal.1:10). “Kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu. Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo.” (1 Wathes.2:4,5).
– Mtumishi wa Mungu HATAFUTI sifa ya watu. “Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine.” (1 Wathes.2:6). 
– Mtumishi wa Mungu HAVITAFUTI vitu vyako … wala faida yake! Anatafuta faida ya kiroho ya waumini.
“Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi…” 2 Wakor.12:14. Maneno ya ajabu! Mtume wa kweli anajitoa kwa ajili ya faida ya kiroho ya washirika!  Paulo alipenda waumini, siyo ‘vitu vyao’! Hatafuti vitu vyao, pesa zao, sifa zao au utukufu kwa watu! Mtumishi wa Mungu anajitoa kwa ajili ya faida ya wale awahudumiao. Anayo nia moja tu, “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.” (2 Wakor.11:2). Naye yupo tayari kujimwaga kwa ajili ya watu wa Mungu ili wapate faida ya kiroho, “Nami kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu. Hata kama kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa.” (2 Wakor.12:15).
Maneno ya kuchanga moto! Mtumishi ya Mungu huzidi kuwapenda waumini awahudumiao hata hivyo anapungukiwa kupendwa!
– Mtumishi anamtegemea Mungu kwa ajili ya mahitaji yake.
“Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; MAANA NIMEJIFUNZA KUWA RADHI NA HALI YO YOTE NILIYO NAYO. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; KATIKA HALI YO YOTE, na katika mambo yo yote, nimefundishwa KUSHIBA NA KUONA NJAA, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” (Wafilipi 4:11-13).
– Mtumishi wa Mungu hufurahi kwa ajili ya waumini wanapotambua ni jambo la haki na la pendo kumsaidia mtumishi ambaye anafanya kazi mbele ya Mungu kwa ajili yao.
“Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi….Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu…. hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. SI KWAMBA NAKITAMANI KILE KIPAWA, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, KATIKA HESABU YENU. Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, HARUFU YA MANUKATO, sadaka yenye kibali, IMPENDEZAYO MUNGU.”
Ndiyo. Paulo alikuwa na mahitaji na alipokea kile kipawa kwa ajili ya MAHITAJI yake (SIYO KWA AJILI KUMFANYA MTAJIRI) kwa furaha – lakini siyo kutokana na uchoyo au tamani yake apate fedha, lakini alifurahi KWA AJILI YA WAUMINI TU. Katika utoaji wao Paulo alitambua matunda ya pendo katika maisha yao ambayo ni kama harufu ya manukato impendezayo Mungu! Alifurahi kwa ajili ya hayo tu! Tena ni wazi hapo kwamba mtumishi wa Mungu hawalazimishi waumini wamtoe pesa. Anafurahi waumini watoe kipawa kwa hiari kutokana na pendo la Mungu mioyoni mwao!
Ni kweli kabisa, na neno la Mungu linatufundisha kwamba ni jambo la haki na la pendo kuwasaidia watumishi wa Mungu SAWASAWA NA MAHITAJI YAO kama wanajitoa kwa ajili yetu. Lakini ndani ya moyo wa mtumishi wa Mungu kwelikweli hamna uchoyo au tamani kwa pesa, kwa sifa, kwa kujiinua, kwa kujifanya mtajiri au kuishi kwa fahari, wala hawalizimishi watu wa Mungu kumpa pesa.
© 2016  David Stamen    somabiblia.com
Read more »

Saturday, May 7, 2016

FAHAMU VYAKULA UNAVYOTAKIWA KULA ILI KUJENGA AFYA YAKO PASIPO GHALAMA KUBWA

Katika sehemu nyingi duniani, watu wengi zaidi hula chakula kikuu chenye bei nafuu ndani ya kila mlo. Chakula hicho kikuu huwapatia nguvu ya kutosha kuwawezesha kutimiza mahitaji yao ya kila siku. Lakini chakula hicho kikuu pekee hakitoshi kumfanya mtu awe mwenye afya. Kuweza kukua, kuwa na nguvu, na kupambana na maambukizi, lazima tule vyakula vingine-zaidi ya chakula kikuu.
Uji ambao haujachanganywa na chochote hautoshi.
Ongezea maharagwe, nyama, maziwa, mayai, mbogamboga,au matunda.


Kwa ajili ya afya bora, tunahitaji:.....BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Read more »

Sunday, May 1, 2016

ROHO YA HEKIMA NA UFUNUO KATIKA KUMJUA YEYE

1
Na: Patrick Sanga

Salaam katika jina lake BWANA Yesu
Katika Waefeso 1:17 Biblia inasema ‘Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi ROHO YA HEKIMA NA YA UFUNUO KATIKA KUMJUA YEYE’. Hili moja ya maombi muhimu ambayo Mtume Paulo alifanya kwa jili ya Kanisa la Efeso. Kila nisomapo mstari huu nimekuwa nikijuliza sana ni kwa nini Mtume Paulo aliomba maombi haya kwa kanisa hili?.
Katika kutafakari na kuendelea kujifunza niligundua kwamba kulikuwa na sababu kubwa tatu ambazo zilimpelekea Mtume Paulo kuwaombea jambo hili, na kutokana na umuhimu wake hata kwa kanisa la sasa ndiyo maana nimeona ni vema nikaliandika hapa ili na wewe msomaji uweze kujifunza.
Zifuatazo ni sababu kadhaa zilizompelekea Mtume Paulo aliombee kanisa la Efeso roho ya hekima na ufunuo na kwa sababu hiyo zinatusaidia kujua umuhimu wake kwa kanisa la sasa pia;
Ili waweze kumjua Mungu zaidi (Waefeso 1:17)
Waefeso 1:11 ‘Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake’.
4
Kazi ya roho ya ufunuo ni kumfunua Mungu kwa kiwango ambacho bado hujakiona wala kukizoea ili kuboresha uhusiano wako na Mungu na kukufanya umaanishe katika kumpenda. Ndiyo, lengo ni kumfunua Mungu kwako, kutoka kwenye kona tofauti tofauti ili umjue zaidi ili hali kazi ya roho ya hekima ni kukupa ufahamu (maarifa), werevu na busara katika kufanya maamuzi sahihi kuhusu uhusiano wako na Mungu na maisha yako kwa ujumla. Katika ufunuo kuna mambo ambayo Mungu atayaleta kwako na yanahitaji hekima katika kuyafasiri, kuyanena na kutenda.
Naam bado hatumjui Mungu kwa kiwango kitupasacho kumjua na ndio maana tunahitaji roho ya ufunuo. Roho ya ufunuo inamuongoza mtu kujenga mahusaino binafsi na Mungu wake tokana na ufunuo aliopata.  Roho hii inatuleta kwenye ufahamu muhimu kuhusu ulimwengu wa roho na kwamba ni lazima tuanze kuishi maisha katika ulimwengu wa roho kuliko vile tunavyoishi katika ulimwengu wa mwili ili kumjua Mungu zaidi.
Ili kujua mambo ambayo Mungu amewaandalia (1Wakorinto 2:9-10)
Katika fungu hilo Biblia inasema hivi ‘Lakini, kama ilivyoandikwa, MAMBO AMBAYO JICHO HALIKUYAONA WALA SIKIO HALIKUYASIKIA, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. LAKINI MUNGU AMETUFUNULIA SISI KWA ROHO. Maana Roho huchunguza yote, hata MAFUMBO ya Mungu’. Pia katika Waefeso 1:18 imeandikwa ‘MACHO YA MIOYO YENU YATIWE NURU MJUE tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo’
5
Mungu anataka watu wake wajue kwamba yeye anayo mawazo (Yeremia 29:11), mbalimbali ambayo amewaandalia watoto wake. Mawazo hayo yameunganishwa na kusudi la kuwepo kwao hapa duniani na hawana budi kuyajua, kuyapata na kuyatenda. Naam ili wafikie hapo sharti juu yao na ndani yao, wawe na roho ya hekima na ufunuo.
Kumbuka katika kila nyanja ya maisha iwe kazi, uchumi, biashara, familia, huduma, ndoa nk, yapo mambo ambayo ameyaandaa na anataka uyajue. Naam ni jukumu lako kuendelea kujenga na kuboresha mahusaino yako na Roho Mtakatifu yawe mazuri daima.
Ili kuujenga mwili wa Kristo ipasavyo
Katika 1Wakorinto 12:7 Biblia inasema ‘Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana’.  Ukiendelea Katika 1Wakorinto 12:20 imeandikwa ‘Na jicho haliwezi kuuambia mkono, sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuaimbia miguu; sina haja na ninyi’ na ule mstari wa 25 unasema ‘Ili kusiwe na faraka katika mwili, BALI VIUNGO VITUNZANE KILA KIUNGO NA MWENZIWE(1Wakorinto 12:25).
Hivyo roho ya ufunuo inatoa ufunuo ili kufaidiana, lengo ikiwa ni kuusaidia mwili wa Kristo kuimarika zaidi. Naam kumbuka ufunuo huu ni kwa sehemu kwa lengo la kulijenga kanisa, mwili wa Kristo. Katika 1Wakorinto 12:11 imeandikwa ‘Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye’. Na tena Mtume Paulo anamalizia kwa kusema ‘Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake’ (1Wakorinto 12:27).
Naam hakuna mtu anayepewa karama zote, kila mmoja anapewa kwa SEHEMU kama KIUNGO ili kwa kushirikiana, MWILI wa Kristo ujengwe vema. Naam kila kiuingo lazima kihakikishe kina kuwa na ufanisi unaotakiwa, si kwa ajii yake, bali kuhakikisha mwili wa Kristo unajengwa ipasavyo, kupitia ufunuo/uwepo wa kile kiungo.
Kanisa lazima lifike mahali pa kuwa na uelewa kamili juu ya mwili wa Kristo unavyopaswa kutenda kazi kupitia ufunuo wa Roho Mtakatifu kwa kuwa ‘Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka (1Wakorinto 12:18). Naam kila mshirika unayemuona NI KIUNGO CHA MWILI WA KRISTO KUPITA KARAMA, VIPAWA NA HUDUMA ALIZOPEWA kwa lengo la kuujenga mwili wa Kristo.  Roho ya hekima ikuongoze kutenda na kujua kwamba karama, huduma na vipawa ulivyonavyo ni kwa ajili ya kuujenga mwili wa kristo.
Naam hatupaswi kumdharau mtu yoyote kutokana na hali yake ya nje kwa jinsi ya kibinadamu maana yeye ni kiungo kinachostahili heshima zaidi (1 Wakorinto 12:22) Kazi ya Mchungaji na viongozi wa kanisa ni kufuatilia ili kujua Mungu ameweka/ametoa/amefunua kitu gani (karama/vipawa/huduma) juu ya wale wanaowaongoza ili kuviendeleza kwa lengo la kuujenga mwili wa Kristo.
3
Hivyo tokana na umuhimu wa roho ya hekima na ufunuo juu ya kanisa la Mungu na kwa mtu mmoja mmoja ni vizuri tukachukua au ukachukua hatua ya kuanza kumomba Mungu akujalie roho ya hekima na ufunuo wewe binafsi, familia yako, jamaa zako na kanisa kwa ujumla ili manufaa yake yawe dhahiri katika mwili wa Kristo ulimwenguni kote.
Roho ya hekima na ufunuo na iwe nanyi
Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA!
cHANZO: Sanga
Read more »

Wednesday, February 3, 2016

The Swedish Church to Collect '39' Million to Build a Mosque

For years the Swedish church parish in Nacka has with an ongoing project planned to build a mosque adjacent to the existing church in Fisksätra in Stockholm. 

The project to build the joint building, called "House of God" is estimated to cost SEK 39 million ($4,548,630), an amount the church tries to collect through a foundation. 

Critics have naturally questioned whether the church really should be building mosques, or instead focus on the Christian faith.

Plans to build the "House of God" in Fisksätra, Nacka municipality in southern Stockholm, began already in 2009. Fisksätra is an ethnic community with a large Muslim populations. The following year, priest and former bishop of Karlstad, Bengt Wadensjö, presented the project in an article in the Swedish newspaper Svenska Dagbladet. He referred to the Sweden Democrats:

Swedish church to collect 39 million to add a mosque- When fear of the unknown in the form of Islam now gives Sweden a profile in the news by SD taking place in parliament, I want to highlight a different picture of Sweden. Jimmie Åkesson (head of SD) wrote in Aftonbladet, October 20, 2009, that "Muslims are our biggest foreign threat". In Nacka we do not believe that immigrants or Muslims would be a threat. They are an asset."

Bengt Wadensjö said that Muslims and Christians should unite in the idea that God is one, and added that "Muslims are generally peaceful and honest", and that the project would lead to that "world peace begins in Fisksätra".

Concretely, the idea is that the mosque will be built next to the church and the two united by a glazed foyer. The Muslim community have been allowed to buy the land needed for SEK 300,000, an amount that will not be paid until the project is complete.

In November 2014, Nacka Parish decided to transfer bequeathed funds to the collection fund to build the mosque, ie money from deceased who wanted to support the Swedish Church by donating money. Although this decision was appealed, the protest was rejected.
Read more »

Tuesday, February 2, 2016

UJUMBE wa Neno la MUNGU


5 Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu akaniweka panapo nafasi.
 6 Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
 7 Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
 8 Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu.
 9 Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu.
 10 Mataifa yote walinizunguka; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
 11 Walinizunguka, naam, walinizunguka; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
 12 Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
 13 Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana akanisaidia.
 14 Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu.
 15 Sauti ya furaha na wokovu Imo hemani mwao wenye haki; Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
 16 Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa; Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
 17 Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya Bwana
(Zab 118:5-17)
UBARIKIWE NA NENO
Read more »
 

Followers


LinkWithin

Hebroni 2016. Powered by Blogger.