SOMO: Uchumba ni nini? na Ndoa ni nini? | Hebroni
Habari Mpya
Loading...

Thursday, January 14, 2016

SOMO: Uchumba ni nini? na Ndoa ni nini?

BONYEZA PICHA HILI CHINI UWE MIONGONI MWA WANAONUFAIKA NA...☟⇓

Shalom, wapendwa,
Katika somo letu leo nataka tuangalie vitu hivi viwili, mahusiano ya uchumba na mahusiano ya ndoa. Sifa za mahusiano ya uchumba na sifa za mahusiano ya ndoa. Kwa nini nataka tujifunze somo hili? Kwa sababu siku hizi za leo kumekuwa hakuna tofauti kati ya uchumba na ndoa, hali hii imeingia mpaka makanisani.
Inashangaza sana, leo wachumba wanafunga ndoa tayari wakiwa wameishakuwa wanandoa, tena wengine wanasubiri wapate watoto wakiwa bado wachumba eti ndio wafunge ndoa. Lakini mbali na hayo, bado namna wachumba wanavyoendesha mahusiano yao yanatafsiri mahusiano ya ndoa, japokuwa ukiwauliza wanasema wao ni wachumba.

Uchumba ni nini, mipaka yake na miiko yake ni ipi? 
Uchumba ni mahusiano ya awali ambayo wawili (mwanamume na mwanamke) ambao bado hawajaingia ktk ndoa wanakubaliana kuoana, na hivyo wanaanzisha mahusiono ya karibu. Makubaliano yao hayo yanaonyesha; 1. Nia yao ya dhati kuwa wanandoa hapo baadae, 2. Maamuzi ya dhati ambayo kila mmoja ameamua kuchukua, na 3. Kwamba kila mmoja amemkubali mwenzake na kwa sababu hiyo anajiandaa kuwa mwenzi wa ndoa wa mwenzake wakati mfupi ujao. Kwa sababu hiyo. Kwa maana nyingine mahusiano ya uchumba ni maandalizi ya pamoja ya mwisho kabla ya ndoa baada ya hawa wawili kujiandaa kila mmoja kwa nafasi na wakati wake. Sasa hapa baada ya kuridhiana kuwa wataoana wanaanza kufanya maandalizi ya pamoja ya mwisho mapema kabla ya ndoa. Kwa hiyo maandalizi ya kuingia ktk ndoa si ndoa. 

Kwa sababu hiyo mtaishi kama kaka na dada kwa kipindi chote cha mahusiano yenu ya uchumba. 

Alama kubwa katika mwenendo wa mahusiano haya ni HESHIMA YA KAKA NA DADA, wakati wote wa mahusiano ya uchumba na si zaidi ya hapo. Zaidi ya hapo, wahusika watajaribiwa kuwa wanandoa wakati wa uchumba wao. Ikumbukwe, uchumba si ndoa, ni mlango utakaowawezesha wawili hawa kwa pamoja wakiwa wamepatana na kukubaliana huku wakiwa kila mmoja amemridhia mwenzake kuingia ktk ndoa kwa agano. Kwa hiyo, uchumba haukuhalalishii kuwa uliyenaye kwenye mahusiano hayo wakati huo ni mume au mke wako. Hivyo, basi, mtakachokuwa mkifanya kwa kipindi chote cha uchumba ni maandalizi ya kuingia ktk ndoa huku kila mmoja akimuheshimu mwenzake kama dada yake au kama kaka yake. Mtatumia Muda huu kupanga mipango ya maisha yenu, kufahamiana kihulka na kitabia, kikubwa zaidi ni kuweka msingi wa ndoa yenu. Kumbuka, hamuwezi kuishi zaidi ya maandalizi mliyoyafanya. Kama hamtajipanga wakati wa uchumba, mkafanya makubaliano ya pamoja ktk baadhi ya mambo au mambo yote yanayowahusu mtashindwana na mtapishana kwa kila jambo wakati wa ndoa. 

Pia, pamoja na kuwa uchumba si ndoa lkn pia sio uwanja wa utakaotumia kuntafuta anayekufaa. Mahusiano haya ni kwa ajili ya wale tu wenye uhakika, waliothibitisha kuwa nitamuoa huyu au nitaolewa na huyu. Na kwa sababu hiyo kama huna uhakika usichumbie, na wala usikubali kuchumbiwa. Kwa nn umuambie mwanamke kuwa unampenda wakati unajua kabisa au huna uhakika kwamba utamuoa.

Au kwa nini umkubalie mwanaume aliyekuambia anakupenda na anataka kukuoa wakati una uhakika kwamba huwezi kuolewa naye au hauna uhakika wa kuolewa naye.

Unapochumbia na unapochumbiwa na ukakubali kusudia kutokuachana, isije baadae ukasema haukuwa mpango wa Mungu, sasa uliingiaje? Bila shaka hukujiandaa. Lkn kumbuka kukosa kwako maandalizi kutasababisha maumivu kwa mwenzako. 

Mtu huingia kwenye mahusiano ya uchumba baada ya kuwa ameishafanya maamuzi, ana uhakika na maamuzi yake, na yuko tayari kuyasimamia kwa gharama yoyote. Usikubali kuachana. Mkisha kubaliana, kuachana Mungu hapendi, anachukia. Kama Mungu hapendi kuachana, basi kila unapoachana na mwenzi wako anachukia. Jiulize, Mungu amechukia mara ngapi kwa upande wako, umeachana mara ngapi na wewe ukiwa ndio sababu? 

Tuangalie Kuhusu Ndoa japo kwa sehemu tu. 
Ndoa ni agano lenye kusudi la wawili (Mwanamume na mwanamke) kuishi pamoja kama mwili mmoja maisha yao yote baada ya kukubaliana, kila mmoja akimkubali mwenzake kuishi na kuwa naye wakati wote ktk hali zote kwa moyo wake wote.
Katika ngazi hii ya mahusiano ndipo watu huwa mke na mume kwa kuunganishwa na Mungu kuwa mwili mmoja. Na ktk ngazi hii tendo la ndoa uhusika, na mambo yote ya faragha yahusuyo upendo, na si ktk uchumba. Huwezi kuishi maisha ya ndoa wakati wa uchumba; ukashiriki tendo la ndoa, na kufanya mambo ya faragha ya upendo na yale yasiyo ya faragha lkn yanawahusu zaidi wana ndoa. Kufanya hivyo ni kuharibu ndoa yenu, lkn kuhatarisha mahusiono yako ya uchumba. 

Unaposhiriki mambo ya ndoa wakati wa uchumba unajijengea na unamjengea mwenzi wako tabia ya kukosa uaminifu ktk ndoa yenu na hivyo kuwa wachepukaji wakati wa ndoa. Lakini pia kufanya hivyo ni kumpa ibilisi nafasi ktk uchumba wenu, na lazima ataharibu tu, asipoharibu kwenye uchumba ataharibu kwenye ndoa, hawezi kuwaacha ivi hivi ikiwa mmempa nafasi. Na kati ya watu wanatumia nafasi bila kupoteza iwapo wataipata, ni shetani. Kwa hiyo kuwa mwangalifu sana. 
Usipoteze uzaliwa wako wa kwanza na mbaraka wako kwa kipande cha mkate ambacho utamu wake haudumu kinywani na ujazo wake haujazi tumbo milele. Japokuwa ni kitamu kitatupwa chooni na wala hutabaki chooni ukifurahi kukitazama. Jitunze, mtunze mwenzi wako, tunza uchumba wako, tunza ndoa yako. Matunzo yanaanza kwa wewe kujitunza, kumtunza mwenzi wako, kutunza uchumba wako na hatimaye kutunza ndoa yako. 

Ubarikiwe na Bwana, 
Wako, Mch. Ezekiel P. Bundala

Crdit>Kanisa Forum

Jiunge Nasi Tuwe Tunakutumia Habari Mara tu zinapotokea! ..Bofya HAPA Ujiunge Sasa..

BONYEZA PICHA HILI CHINI UWE MIONGONI MWA WANAONUFAIKA NA...☟⇓
Sambaza Habari Hii Kwa Marafiki Zako
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
ANGALIA TV KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI
Bofya HAPA>>HAPA>>HAPA

0 comments:

POST A COMMENT

 

Followers


LinkWithin

Hebroni 2016. Powered by Blogger.