BONYEZA PICHA HILI CHINI UWE MIONGONI MWA WANAONUFAIKA NA...☟⇓
Mtajiri na maskini anaweza kujitoa:
2 Kor 8:1-5
Baadhi ya makanisa yalikuwa yameamua kuwasaidia wakristo wa Yerusalemu waliopatwa na shida ya njaa. Paulo anawaandikia Wakorintho akiwataja Wamakedonia kama mfano mzuri wa kujitoa. Wamakedonia walikuwa hawana mali nyingi. Wenyewe waliishi kwa shida. Hata hivyo walitoa hata kupita uwezo wao ili wasaidie wenzao huko Yerusalemu. Paulo anasema walijitoa nafsi zao kwanza kwa Bwana, na hata kwa ndugu zao katika imani.
2 Kor 8:7
Wakorintho ambao walikuwa hawakosi kitu waliambiwa watoe kwa ukarimu. Wajitoe wenyewe kama Wamakedonia walivofanya.Yesu ni mfano mkuu wa kujitoa:
Rum 15:3
2 Kor 8:9
Fil 2:4-8
Yn 3:16
Kujitoa inamaanisha kujali mahitaji ya wengine. Usifikirie mahitji yako mwenyewe tu. Huenda mwenzako ana mahitaji makubwa kuliko wewe. Jirani yako huenda anapotea katika dhambi wakati wewe unatafuta mali ya dunia hii. Yesu alikuwa ana kila kitu alipoishi mbinguni, lakini akaamua kuzaliwa horini kama mtu maskini, na akafa msalabani ili sisi tusipotee.Kwa nini tujitoe?
Fil 2:9-12
Kwa ajili ya kujitoa kwake Yesu Mungu akamwinua juu ya yote. Kwa nini Mungu akafanya hivyo?
Yn 12:24
Sheria ya kiroho inasema; Ili uhai upatikane, lazima kifo kiwepo kwanza. Unapojitoa kwa Mungu maisha yatakuwa yenye maana zaidi. Usipojitoa na moyo wako wote huenda utapotea, au utaokoka kwa neema, lakini utabaki kama mbegu pekee isiopandwa ardhini. Mbegu ikipandwa ardhini inazaa. Unapojitoa mia kwa mia unapandwa kama mbegu ardhini. Kwa namna fulani unakufa, lakini utazaa matunda. Mimi binafsi ninaomba nikifika mbele za Mungu siku moja nije pamoja na watu waliomwamini kwa sababu ya kujitoa kwangu.Faida za kujitoa:
2 Kor 9:6-8
Faida ya kwanza: Mahitaji yako ya kila siku utayapata
Anayetoa mali, muda wake, nguvu zake na moyo wake wote kwa furaha na kwa hiari yake mwenyewe ameahidiwa kwamba mahitaji yake ya kila siku atayapata. Na Mungu anajaza kikombe chake mpaka kinafurika. Anapewa uwezo wa kutoa tena, na ngurudumu ya baraka kwake na kwa wengine inaanza kuzunguka.
2 Kor 9:13-14
Faida ya pili: Watu watakuombea.
Ukijitoa kwelikweli kwa Bwana utakuta watu wengine wanabarikiwa. Haitakuwa vigumu kwao kukukumbuka wanapomwomba Mungu. Mtu anayeombewa na wenzake anapata ushindi hata anapopita katika magumu maishani.Faida ya tatu: Jina la Bwana litasifiwa.
Mkristo alieokoka ana lengo moja tu: kumtumikia Mungu. Mtu anapojitoa jina la Bwana linasifiwa. Ufalme wa Mungu unaenea. Mkristo wa kweli ataona hii ni faida kubwa sana.Jiunge Nasi Tuwe Tunakutumia Habari Mara tu zinapotokea! ..Bofya HAPA Ujiunge Sasa..
BONYEZA PICHA HILI CHINI UWE MIONGONI MWA WANAONUFAIKA NA...☟⇓
0 comments:
POST A COMMENT